RODGERS KUMPISHA ANCELOTTI LIVERPOOL

RODGERS KUMPISHA ANCELOTTI LIVERPOOL

BURUDANI - - MBELE -

HII imekula kwake! Kocha Brendan Rodgers anapambana kuokoa kibarua chake, baada ya wamiliki Kampuni ya FSG kutaja jina la Carlo Ancelotti ili kutwaa mikoba yake.

Ancelotti, ambaye alitwaa Kombe la Ulaya na AC Milan na Real Madrid, amerushiwa ndoano ya kumrithi Rodgers baada Liverpool kuanza msimu vibaya.

Inafahamika kwamba Rodgers anakingiwa kifua na baadhi ya maofisa wanaotoa uamuzi Liverpool, lakini kibarua chake sasa kipo shakani baada ya Ancelotti kupigiwa simu ili kuziba nafasi hiyo.

Rodgers ameanza msimu vibaya na matokeo yao hivi karibuni, sare 1-1 na timu ya Norwich City, yanamweka kocha huyo wa Liverpool kitanzini.

Kufungwa mabao 3-0 katika uwanja uwanja wa nyumbani wa Anfield na West Ham, na kupigwa dhidi ya Manchester Uinted, vichapo hivyo vimeshatosha kuishawashi FSG kutafuta mbadala wake.

Ancelotti ana wasifu mzuri kufuatia kuipa mataji mawili Chelsea baada ya kujiunga nao kutoka AC Milan.

Kwa sababu hiyo Liverpool inaamini anafaa kupewa mikoba kutokana na kuongoza timu nyingi kwa mafanikio.

Aidha, Ancelotti siku zote amekuwa akivutiwa kuinoa klabu hiyo ya Anfield.

“Nimeifuatilia Liverpool tangu 1984 baada ya kucheza nao na Roma katika fainali ya Kombe la Ulaya, tulipofungwa kwa penalti,” alisema mwaka jana.

“Ni klabu inayonivutia. Wanaimba vizuri ìKamwe hutatembea mpweke”. hakuna anayeweza kuimba kama mashabiki wa Liverpool.”

Kocha huyo raia wa Italia pia aliiongoza timu ya Paris SaintGermain kutwaa ubingwa wa ligi ya Ufaransa kabla ya kuajiriwa na Real Madrid, ambapo aliandika historia kwa kuipa taji la 10 la klabu bingwa Ulaya.

JOHN

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.