Msumi ashtuka

BURUDANI - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

MWENYEKITI wa Matawi ya Klabu ya Yanga, Mohamed Msumi, amesema kwamba wameshtukia njama za wapinzani wao Simba.

Msumi alisema hayo jana, wakati akizungumza na Burudani jijini Dar es Salaam kuwa wameitegua mipango yote ya wapinzani wao.

Alisema, miongoni mwa njam hizo ni kutaka kuwachunguza mahali ambapo wameweka kambi kujiandaa na mchezo huo.

“Hawa jamaa wamekuwa wakijaribu kutufutilia tunafanya nini kwenye kambi yetu,mambo yote tumebaini na tumepangua, hawawezi kupata kitu,safari hii tumemtega vizuri mnyama hawezi kupenya,” alisema Msumi.

Yanga imeweka kambi yao Pemba huku Simba wao wakiwa wameweka kambi Unguja kwa ajili ya kujiandaa na mpambano huo ambao unavuta hisia kwa mashabiki wa soka.

MOHAMED Msumi

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.