Kiiza akiri mchezo mgumu

BURUDANI - - HABARI - NAMWANDISHI WETU

MSHAMBULIAJI wa timu ya soka ya Simba, Hamis Kiiza amesema kuwa, mchezo wa Yanga na Simba ni mgumu kwa kila upande.

Kiiza alisema hayo hivi karibuni, kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, kuwa ana imani mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa.

“Kweli mchezo utakuwa mgumu kwa kila upande, lakini tutakwenda kupambana ili kuwamaliza hao Yanga na kuchukua pointi tatu,” alisema.

Hata hivyo, mchezaji huyo ambaye ni raia wa Uganda, amewaomba waamuzi ambao watachezesha mpambano huo kuzingatia sheria 17 za soka ili mshindi aweze kupatikana kwa haki.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.