Mieleka ya Nyerere yakwama

BURUDANI - - HADITHI/KATUNI - NA MWANDISHI WETU

MICHUANO ya Kombe la Hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere, ambayo ilipangwa ifanyike kuanzia Oktoba 14, mwaka huu mkoani Dodoma sasa haitafanyika.

Akizungumza hivi karibuni kwa njia ya simu kutoka Bagamoyo, Pwani, Katibu Mkuu wa Chama cha Mieleka Tanzania (AWATA), Vicent Magesa alisema hali hiyo imetokana na klabu nyingi shiriki wachezaji wake wengi wanatoka katika taasisi za majeshi ya Ulinzi na Usalama.

Alisema hivyo wachezaji hao ni waajiriwa wa taasisi hizo, alisema katika muda huo hawatakua na fursa ya kushiriki michuano hiyo kutokana na majukumu mazito ya uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ambao utafanyika Oktoba 25.

“Ni kweli kuwa tulipanga kufanya mashindano maalumu kwa ajili ya kumbukumbu ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania, Hayati Nyerere baadaye mwezi huu huko Dodoma, lakini sasa mashindano hayo hayatafanyika tena,” alisema Magesa.

Katibu huyo, alisema badala yake michuano hiyo, alisema sasa itafanyika mwakani na kuzitaka klabu kujipanga upya kwa ajili ya tukio hilo mwakani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.