Samata,Ulimwengu hawakamatiki

BURUDANI - - HABARI - NA NASRA KITANA

TIMU ya Taifa (Taifa Stars),jana imewapa raha baada ya kuichapa kwa mabao 2-0 timu ya Taifa ya Malawi katika Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam,mchezo huo wa kusaka nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia,zitakazo fanyika mwaka 2018 nchini Russia.

Stars ilianza mchezo huo kwa kasi ambapo dakika ya pili,Shomari Kapombe alipanda na mpira na kupiga mpira wa krosi iliyomkuta Mrosho Ngasa lakini alishindwa kufunga baada ya kuzongwa na walinzi wa Malawi.

Mbwana Samata alipachika bao la kuongoza dakika ya 18 baada ya kupewa pasi nzuri na Thomas Ulimwengu ambapo walionekana kuisumbua sana ngome ya timu ya Malawi katika mchezo huo.

Kasi ya Stars ilizidi kuwa kubwa ambapo dakika ya 22 ya mchezo huo,Ulimwengu alifunga bao la pili baada ya kupokea mpira wa krosi kutoka kwa Haji Mwinyi.

Malawi nao walifanya shambulizi dakika ya 37, baada ya kipa Ali Mustapha ‘Barthez’kudaka shuti kali lililofumuliwa na John Banda.

Taifa Stars nao walifanya shambulizi la nguvu dakika ya 43 baada ya Farid Musa kupanda na mpira na kisha kupiga krosi iliyomkuta Ulimwengu ambaye alikosa bao.

Dakika ya 55 Ulimwengu alipanda na mpira na kumpa pasi safi Mrisho Ngasa ambapo alikosa bao kwa kichwa baada ya kupiga nje ya lango la Malawi.

Stanley Sanudi anapewa kadi ya njano dakika ya 72 na mwamuzi wa mchezo huo,Hagi Yabarow Wiish baada ya kumfanyia madhambi Farid Musa wa Taifa Stars.

Malawi walikosa bao dakika ya 80Isaac Kaliati kupiga shuti kali ambalo liliokolewa na kipa Ali Mustapha ‘Barthez’.

Taifa Stars: iliwakilishwa na Ali Mustapha,Shomari Kapombe,Haji Mwinyi,Nadir Haroub,Kelvin Yondan, Himid Mao,Thomas Ulimwengu/Ibrahimu Ajibu, Said Ndemla, Mbwana Samata, Mrisho Ngasa/ Salum Telela na Farid Musa/ Saimon Msuva.

Malawi: Simplex Nthala, Stanley Sanudi, Mivale Gabeya, Yamkani Fadya, Limbikani Mzava, Gerald Phiri/Isaac Kaliati, Chimango Kayira, Micium Mhone/Mamase Chiyasa, Chawangiwa Kawanda,John Banda/ na Robin Ngalande/ Gabadinho Mhango.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.