Muro: Tutawashangaza Azam

BURUDANI - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

UONGOZI wa klabu ya Yanga,umetamba kuwa utawashangaza Azam FC kwa kuwachapa mabao kwenye mchezo wa Ligi Kuu.

Tambo hizo,zimetolewa jana na Ofisa Habari wa klabu hiyo, Jerry Muro wakati akizungumza na Burudani kwamba wanaendelea kujipanga ili kuwashangaza wapinzani wao katika mchezo utakao fanyika Unwanja wa Taifa,Dar es Salaam.

Alisema wameanza kazi hiyo kimya kimya ili kuhakikisha wanachukua pointi tatu na kuzidi kuongoza ligi hiyo ambayo amekiri kwamba msimu huu ina ushindani mkubwa.

“Tupo makini kwa ajili ya kupambana na Azam FC, kazi hiyo itafanyika kimya kimya kama tunamkimbiza mwizi,lakini itakuwa kubwa kuliko ilivyokuwa dhidi ya Simba ambao wapo kwenye kisigino cha mguu huko,”alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.