SPUTANZA yajipanga upya

BURUDANI - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

CHAMA Cha Wachezaji Nchini (SPUTANZA),kimetoa tamko kwamba kipo mbioni kuanza kutoa mafunzo ya saikolojia kwa wachezaji ili waweze kujitambua.

Mwenyekiti wa chama hicho,Musa Kisokyi alisema jana kuwa wameanza kazi hiyo kwa kufanya mazungumzo na baadhi ya madaktari ili waweze kuweka utaratibu wa kufanya hivyo.

Alisema lengo lao ni kutaka kuwapa mafunzo wachezaji waweze kujifahamu kwa vile ni kioo cha jamii na hawapaswi kufanya mambo yasiyo takiwa kwa jamii.

“Unajua yapo baadhi ya mambo wachezaji hawapaswi kufanya kwenye jamii yetu,lakini nafikiri kazi hiyo itaweza kukamilika siku chache zijazo na wachezaji wakaweza kupewa mafunzo ili kuwaondoa kwenye matatizo,”alisema.

Kauli ya kiongozi huyo,imekuja siku chache baada ya Nahodha wa timu ya Mbeya City,Juma Nyoso kufungiwa miaka miwili na kutozwa faini ya Shilingi milioni mbili baada ya kufanya kitendo cha udhalilishaji

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.