Micho abadili mfumo wa mazoezi

BURUDANI - - AFRIKA -

KAMPALA, UGANDA

EMMANUEL Rubona

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifaya

Uganda Cranes, Sredojevic Milutin ‘Micho’, amesema anapenda kutumia dakika 60 kuwapa mazoezi ya nguvu wachezaji wa timu hiyo.

Micho alisema hayo juzi, kwamba amepanga kubadili mfumo wa mazoezi wa kikosi chake, alisema ili kiweze kuwa na kasi ya kusaka uashindi uwanjani.

Alisema uamuzi huo umekuja baada ya kugundua wachezaji wengi wanaounda timu hiyo, alisema wapo fiti kutoka kwenye timu zao.

“Mimi kazi yangu ni kuwapa mazoezi ya nguvu ndani ya dakika 60, ambazo nina imani zinaweza kuwaweka fiti,”alisema kocha huyo.

Hata hivyo, kocha huyo amesema bado ana kazi kubwa ya kuunda mfumo wa ushambuliaji kwenye timu yake hiyo, alisema ili hatimaye iweze kufanya vyema katika mechi zake.

BENCHI la ufundi la timu ya soka ya APR ya Rwanda, limetamba kikosi chao kimeanza kuimarika kadri kinavyozidi kucheza mechi mbalimbali.

Tambo hizo, zimetolewa na kocha mkuu wa timu hiyo, Emmanuel Rubona, kwamba kikosi chake kwa sasa kimeanza kazi.

Alisema lengo lao msimu huu ni kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini humo ili msimu ujao waweze kuiwakilisha nchi yao kwenye mashindano ya kimataifa.

“Tupo makini, tulianza vibaya lakini nashukuru wachezaji wangu wameanza kuelewa mfumo ambao ninataka wacheze, tunataka kuchukua ubingwa kwa mara ya 16, kama tutafanikiwa,” alisema kocha huyo.

Kauli hiyo,imekuja siku chache baada ya APR kucheza mzunguko wa tano wa michuano hiyo ambapo hivi sasa ina pointi 10 ikiwa ya tatu.

Timu ambayo inaongoza ligi hiyo ni AS Kigali ambapo ina pointi 15, ikifuatiwa na timu ya Polisi ambayo ina pointi 12 lakini kocha huyo ametamba kuwa ana imani watakuwa juu ya msimo muda mfupi ujao.

“Wachezaji wangu wapo makini, sasa tuna kila sababu ya kufanya vizuri kwenye mechi zote zijazo ilikutimiza wazo la kuchukua ubingwa msimu huu,hakuna timu ya kutuzuia,”alisema kocha huyo.

SREDOJEVIC Milutin ‘Micho’

JOHNNY McKinstry

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.