MATUMAINI MAPYA

MESUIT Ozil akishangilia bao aliloifungia Arsenal juzi

BURUDANI - - MBELE -

ARSENAL juzi, iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Bayern Munich katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa ulaya, lakini imejikuta ikimpoteza nyota wake Aaron Ramsey.

Mshambuliaji huyo alipata majeraha alipokuwa akiipigania timu yake kwenye mchezo huo wa ushindani, ambao umeonyesha matumaini mapya kwa Arsenal.

Katika mchezo huo uliochezwa uwanja wa Emirates, Arsenal walitandaza kabumbu la uhakika na kujiweka pazuri katika kundi F.

Kuumia kwa Ramsey, kutaifanya Arsenal kumkosa mshambuliaji huyo katika mchezo ujao wa ligi kuu ya England dhidi ya Everton.

Lakini, Wenger raia wa Ufaransa, anafikiria kumpumzisha Alex Sanchez baada ya kumtumia katika michezo mingi. Anaamini mshambuliaji huyo amechoka, angehitaji kupumua.

“Aaron Ramsey yuko vizuri, lakini aliniambia ana maumivu ya misuli kwake itakuwa ngumu kucheza. Atakuwa nje,” alisema Wenger.

Mabao ya Olivier Giroud na Mesut Ozil yalitosha kuipa Arsenal matumaini ya kusonga mbele katika michuano ya ligi ya mabingwa.

Nayo Barcelona ikicheza bila nyota wake, Lionel Messi iliibanjua BATE Borisov mabao 2-0.

Bao la kwanza la Barca, liliwekwa kwenye kamba na Ivan Rakitic alilofunga dakika ya 48.

Mfungaji huyo alionekana nyota katika mchezo huo, kwani dakika 16 baadae, akaiandikia Barcelona bao la ushindi na kuzima ndoto za BATE kushinda uwanja wa

nyumbani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.