Madrid yamkomalia Sanchez

BURUDANI - - HABARI -

MADRID, HISPANIA

TIMU ya Real Madrid, imefanya tena mazungumzo na Arsenal kutaka kumsajili nyota wa timu hiyo, Alexis Sanchez.

Madrid imekuwa ikihaha kutaka kumsajili mchezaji huyo ili kuongeza nguvu katika kikosi hicho.

Klabu hiyo inamni kwamba itamshawishi nyota huyo kujiunga ili atwae mataji baada ya Arsenal kushindwa kutwaa tangu mwaka 2004.

Sanchez( 26) msimu uliopita alicheza michezo 52 na kupachika mabao 25.

JAMIE Vardy

LONDON, England

KOCHA mkuu wa timu ya Leicester City, Claudio Ranieri, amesema hakuna timu yoyote inayoshiriki Ligi Kuu England yenye uwezo wa kumsajili nyota wake, Jamie Vardy.

Ranieri anaamini kwamba mchezaji huyo atajiunga na Real Madrid wakati wa dirisha la usajili.

Vardy ameonyesha kiwango bora na kufanikiwa kuongoza orodha ya wafungaji baada ya kupachika mabao 10.

Tayari timu mbalimbali zimeanza kurusha ndoano kwa ajili ya kutaka saini ya nyota huyo wakati wa dirisha la usajili Januari.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.