DK. CHENI ALALAMIKIA UGUMU WA SOKO

BURUDANI - - WAZO -

RAPA wa muziki wa kizazi kipya, Erick Msodoki ‘Young Killer,’ ameamua kutafuta msimamizi wa kazi zake kwa ajili ya kumsaidia kama ilivyo kwa wasanii wengine.

Amesema siku zote msimamizi ni muhimu, kwani unakuwa na muda wa kufanya kazi nyingi na nzuri kwa ushauri kutoka kwake.

Akizungumza na safu hii Dar es Salaam, Killer alisema binafsi alikuwa anashindwa kufanya vizuri kutokana na kukosa msimamizi makini kwa sababu kazi zake zote anazifanya mwenyewe.

“Kama kuna mtu anaweza kuwa msimamizi wa kazi zangu, ajitokeze ili tuweze kukaa chini na kupanga jinsi ya kufanya kazi,”alisema

Alisema kwa sasa ameona umuhimu wa kuwa na msimamizi kwani amekuwa na kazi nyingi.

MKONGWE wa filamu nchini, Muhsein Awadh ‘Dk. Cheni,’ amesema wasanii wako wengi, hivyo kuna changamoto kubwa ya masoko.

Amesema kwa kawaida, ana uwezo wa kutoa kazi nyingi kwa mwaka, lakini anashindwa kufanya hivyo kutokana na mazingira yaliyopo.

Akizungumza na safu hii jana Dk. Cheni alisema, tatizo la usambazaji bado ni kilio kwa wasanii nchini na wasipokuwa makini, hali itakuwa mbaya.

“Inabidi wasanii wa filamu tushikamane kuhakikisha tunamaliza masuala hayo, kazi zetu ziweze kupata soko na wasambazaji makini,”alisema

Aliwataka wasanii wote nchini, kushikamana kuwa kitu kimoja ili kuhakikisha wanaishinda hali hiyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.