Mexime: Tutapambana hadi mwisho

BURUDANI - - HABARI -

KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Meck Mexime, amesema kikosi chake kinahitaji kuboreshwa ili kiweze kupata matokeo mazuri zaidi.

Mexime, amesema ana uhakika wa kumaliza vyema michuano ya Ligi baada ya kupata matokeo mazuri katika michezo iliyopita.

Alisema timu yake imepoteza mchezo mmoja dhidi ya Yanga kwa mabao 2-0 kwenye uwanja wa Jamhuri, lakini bado ana uhakika wa kushika nafasi za juu.

Akizungumza kwa njia ya simu, Mexime, alisema timu yake inahitaji maandalizi na kuongeza mbinu ili iendelee kukaa katika nafasi za juu.

Alisema ushindani msimu huu ni mkubwa kwani timu zote zimejiandaa vyema hivyo amepanga kufanya marekebisho ili kuendelea kubaki katika nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi.

“Tuna kazi kubwa ya kuhakikisha tunamaliza katika nafasi nzuri, hakuna timu mbovu kila timu imejipanga inataka pointi tatu, cha msingi tunapaswa kuongeza nguvu ili tumalize vyema,” alisema Mexime.

Kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Kagera Sugar, Mtibwa ilikuwa nafasi ya tatu ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza michezo saba.

Mecky

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.