Kocha Sports aigwaya Prisons

BURUDANI - - HABARI -

KOCHA mkuu wa African Sports, Joseph Lazaro, amesema mchezo dhidi ya Prisons utakuwa mgumu.

African Sports, inatarajia kushuka dimbani leo kwenye uwanja wa Sokoine kuvaana na Prisons katika mchezo wa raundi ya nane ya ligi kuu.

Prisons itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba katika mchezo uliopita uliofanyika kwenye uwanja huo.

Akizungumza kwa njia ya simu, Lazaro, alisema mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na morali ya wapinzani wao.

Alisema Prisons wana morali kubwa baada ya kupata ushindi katika mchezo uliopita.

“Kwa kutambua ushindani tutakao kutana nao tumejiandaa vyema, ili kuhakikisha tunapata pointi tatu,”alisema mchezaji huyo wa zamani wa Simba.

African Sports inashika nafasi ya pili toka mkiani ikiwa na pointi tatu baada ya kushuka dimbani mara saba imeshinda mechi moja, na imepoteza michezo sita.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.