Kerr alia na nyasi za taifa

BURUDANI - - HABARI - NA GULE MANDAGO

KOCHA mkuu wa Simba, Dylan Kerr, ameponda nyasi za uwanja wa taifa kuwa ni ndefu na zinasababisha wachezaji washindwe kupiga pasi za uhakika.

Kerr amekuwa akilia na nyasi hizo kwamba hazina ubora kwa sababu ni ndefu na zinasababisha wachezaji kushindwa kufanya kile anachotaka.

Akizungumza na gazeti hili, Kerr, alisema uwanja wa taifa ni mbovu kutokana na nyasi zake kuwa ndefu ukilinganisha na viwanja vingine.

Alisema uwanja huo umepoteza hadhi na unahitaji marekebisho kwani unakwamisha makocha.

“Huwezi ukalaumu mchezaji, kwani viwanja vyenyewe ni vibovu kupindukia, mpira hautulii si viwanja vya mikoani hata uwanja wa taifa nao una nyasi ndefu sana, wenzetu nyasi zinakuwa ni ndogo na zinafanyiwa marekebisho kila wakati,”alisema Kerr.

Alisema wachezaji wanashindwa kucheza vizuri kutokana na viwanja kuwa vibovu.

“Viwanja vinapaswa kuwa katika viwango ambavyo vinatakiwa huwezi ukacheza katika uwanja ambao hauna vigezo na kufanya hivi ni kuumiza wachezaji,” alisema kocha huyo.

mipango

ya

UONGOZI wa timu ya Azam FC,umesema Simba na Yanga zinatafuta sababu baada ya kuona kikosi chao kipo imara na

kudai ratiba ya Ligi Kuu kamwe haiwabebi isipokuwa imeangalia baadhi ya vigezo ikiwemo kuonesha moja kwa moja na

kituo cha Luninga cha Azam TV.

Mkurugenzi Mtendaji wa timu hiyo, Saad Kawemba, alisema kwamba baadhi ya michezo imekuwa inatofautiana na timu

nyingine kutokana na kuwepo shinikizo kutoka kwa wadhamini.

Alisema alisema haiwezekani michezo yote ikachezwa siku moja ikizihusisha timu za Simba,Yanga na Azam kwa vile

mdhamini ana penda kuonesha michezo hiyo.

“Zipo sababu nyingi za msingi,kwanza matakwa ya wadhamini wa ligi hiyo,pili mazingira,kuna baadhi ya sehemu timu

ikienda inabidi isiburi siku kadhaa ili iweze kucheza mchezo unaofuata kukwepa gharama ya usafiri,malazi na mambo mengine,” alisema. Kauli hiyo,imekuja siku chache baada ya viongozi wa Yanga na Simba kudai kwamba kuna mbinu zimepangwa kuipa

nafasi Azam FC kutwaa ubingwa wa ligi hiyo msimu huu.

Katibu Mkuu wa Yanga,Dk. Jonas Tiborohoa alisema kwamba wao wanashangaa kwanini mechi zao zinatangulia kufanyika

halafu Azam inacheza siku inayofuata kitu ambacho alisema kuna uwezekano wa kuandaliwa mazingira ya ubingwa.

Naye Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amekiri kuwepo kwa hali hiyo na kusema wao wana wasiwasi kuna mbinu

zimepangwa kuiwezesha Azam kuwa bingwa.

Mwenyekiti wa Kusimamia Bodi ya Ligi Kuu, Ahmad Yahya,alisema bodi yake haina mpango wa kuibeba timu yoyote

katika michuano hizo na kueleza kuwa sababu hizo hazina msingi wowote.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.