Kiiza: Nitapambana hadi kieleweke

BURUDANI - - HABARI -

MSHAMBULIAJI wa Simba, Hamis Kiiza, amesema kwamba hajakata tamaa kupigania kiatu cha dhahabu msimu huu.

Akizungumza na gazeti hili, Kiiza alisema bado ana nafasi ya kupigania kiatu hicho endapo atapata nafasi kucheza katika kikosi hicho.

Alisema mbio za kuwania kiatu hicho zimeshika kasi kutokana na ushindani uliopo kati ya Donald Ngoma wa Yanga na Elius Maguri wa timu

ya ya Stand United.

Maguri anaongoza mbio hizo baada ya kupachika mabao tisa, akifuatiwa na Donald Ngoma ambaye amefunga mabao nane.

“Nilikuwa majeruhi na ninamshukuru Mungu nimerejea na kasi ile ile,nitaendelea kujituma katika mazoezi na kusikiliza maelekezo ya kocha, pia kipindi hiki Ligi imesimama nadhani ni wakati mzuri wa kujifua ili niweze kuwa fiti ,”alisema Kiiza.

Michuano ya Ligi Kuu Bara raundi ya 11 inatarajiwa kuendelea tena Desemba 12,

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.