Lunyamila wa Twiga Stars apewa ulaji

BURUDANI - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

Chabruma

MARTIN Glerics

UONGOZI wa Klabu ya Toto Africans ya Mwanza, umekiri Kocha wao Mkuu, Martin Glerics kutoka Ujerumani amekimbia kutokana na ukata unaoikabili timu hiyo.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Godwin Aiko, alisema jana kutoka mkoani Mwanza, alisema kocha huyo aliondoka hivi karibuni mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC uliyofanyika wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Azam Complex, uliyoko Chamazi, Dar es Salaam.

Alisema kocha huyo ameamua kuondoka baada ya kugundua baadhi ya mambo , alisema yamekwenda tofauti na alivyokuwa anafikiria mara ya kwanza kabla ya kuingia mkataba wa kuinoa timu hiyo kwa miaka miwili.

“Ni kweli kuwa kocha Glerics ameondoka na amekwenda kwao. Amesema kama tutarekebisha hali ya ndani ya klabu atarudi. Ila kwa sasa tuna makocha watatu ambao wataendelea na kazi,” alisema Mwenyekiti huyo.

Aliongeza, timu hiyo sasa itabaki na kuwa chini ya John Tegete ambaye atakuwa kocha mkuu, ambaye atasaidiwa na makocha wengine wawili kwa ajili ya michuano ya ligi kuu msimu huu. SHAMBULIAJI wa timu ya soka ya taifa ya Wanawake, Twiga Stars, Ester Chabruma atajiunga na benchi la ufundi la timu hiyo mara atakapostaafu kuichezea timu hiyo.

Taarifa iliyopatikana jana, imeeleza kuwa uamuzi huo umekuja siku chache baada ya nyota huyo kueleza nia yake ya kustaafu kuichezea Twiga.

Mchezaji huyo ameichezea muda mrefu timu hiyo, kabla ya kufikia uamuzi wa kustaafu kukichezea kikosi hicho ambacho Jumamosi kitaivaa timu ya taifa ya wanawake ya Malawi.

Mchezo huo ambao ni wa kimataifa wa kirafiki, utafanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, uliyoko Chamazi, Dar es Salaam.

Hata hivyo, mkali huyo amesema ataendelea kushirikiana na viongozi wa benchi la ufundi la Twiga, alisema ili kuwapa uzoefu wake wachezaji watakaoendelea kuichezea timu hiyo.

“Kweli nimepewa taarifa hiyo, wakati wowote itatangazwa rasmi na mimi kwa ukweli nimefurahi kuichezea muda mrefu nchi yangu,” alisema mchezaji huyo ambaye anafananishwa kasi yake kiwanjani na mchezaji wa zamani wa Yanga, Edibily Lunyamila.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.