Anahesabu siku Chelsea

BURUDANI - - HABARI -

Bila kuficha, maneno hayo yataleta ukakasi kwa mmiliki wa klabu hiyo, Abramovic, benchi la ufundi, wanachama na mashabiki kwa ujumla. Lakini hayapaswi kupuuzwa kwani mwanzo wa jipu ni kipele.

Richardson anasema uhusiano wa Mourinho na wachezaji wake si mzuri ndio maana ari imeshuka katika timu nzima iliyomfanya aringe kutokana na heshima aliyopata alipoanza kibarua chake 2004 na kutimka 2007 kisha kurejea 2013.

Mtangazaji huyo anasema: “Ngoja nikufahamishe kuhusu stori ya Chelsea. Taarifa yangu inatoka kwa mchezaji wa kikosi cha kwanza Chelsea.

“Taarifa hiyo kweli ilinifikia kwa njia ya mawasiliano. Niliambiwa kuwa Jose Mourinho uhusiano wake na wachezaji wengi haupo sawa.

“Nimeambiwa wanachukia jinsi anavyofanya kazi na baadhi yao. Wamechoshwa na anavyowakaripia. Niliambiwa uhusiano wake hasa na Eden Hazard umepungua.”

Aliongeza: “Hapa naanza kunukuu. Mchezaji mmoja alisema hivi karibuni, ‘ Bora nifungwe kuliko kushinda kwa ajili yake’. Nukuu hiyo pengine inasababisha haya yanayosemwa sasa, lakini labda inashusha molari ya baadhi ya wachezaji.”

Mashabiki wa Chelsea wamechukia ukuu hiyo inayolenga kumharibia Mourinho, lakini Richardson amekingiwa kifua na Naibu Mhariri wa kipindi cha 5 Live, Simon Clancy kwamba kilichosemwa ni sahihi.

Kocha huyo amepewa mechi mbili za kuokoa kibarua chake vinginevyo ajira yake itachukuliwa kwa muda na Carlo Ancelotti.

Abramovich, ingawa amejiandaa kumpa muda Mourinho, vyanzo vinasema kura ya imani naye imepungua baada ya Chelsea kufungwa nyumbani na Southampton mapema mwezi uliopita, huku hatima pekee ya Mreno huyo ikipigiwa mstari na tajiri wake kwamba mwisho ni Novemba wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.

Chelsea ikigonga mwamba kwa Dynamo Kiev katika ligi ya mabingwa Ulaya mchezo uliopangwa kufanyika jana na ikitolewa hatua ya makundi, mechi na Stoke City itakayopigwa Jumamosi huenda ikawa ya mwisho kwa Mourinho kufanya kazi katika klabu hiyo.

Bilionea Abramovich anataka kuangalia michezo miwili, ukiwemo uliopigwa Jumamosi ambao Chelsea ilichezea bakora 3-1 nyumbani kwa Liverpool, ndipo atoe uamuzi.

Mtazamo uliotanda katika klabu hiyo ni kama Mourinho amefukuzwa, ingawa mapumziko ya mechi za kimataifa yanaweza kumpa muda wa kujipanga kisha kufanya maajabu na kujitoa katika kitanzi kinachomkabili sasa.

Ingawa Chelsea hawana mawasiliano ya moja kwa moja na Ancelotti, mazungumzo yameshafanyika na washauri wake.

Wawakilishi hao wa kocha huyo Mtaliano wameonyesha kuvutiwa na ‘dili’ hilo, hata kama la muda mfupi kwani litakwisha mwisho wa msimu huu.

Ancelotti, ambaye aliinoa Chelsea kati ya mwaka 2009 na 2011, na kushinda mataji mawili binafsi anatafsiriwa kwamba ni miongoni mwa watu waliopata wakati mgumu sana katika nyakati alizofanya kazi kwenye klabu hiyo na anatamani kurudi pasipo wasiwasi wowote.

Pamoja na magumu hayo Mourinho amesema mashabiki wa Chelsea wanampa faraja kutokana na kuimba jina lake.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.