Khloe Kardashian: Ukibwia unga utakiona

BURUDANI - - WAZO | HOJA -

LOS ANGELES,Marekani MREMBO Khloe Kardashian, amemchimba mkwara mzito mumewe Lamar Odom, kuwa akirudia kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume atamkomesha.

Khloe alisema jana kwamba amevumilia kwa muda mrefu tabia ya mumewe na sasa inabidi abadilike na kuwa mkali.

Alisema kitendo cha Odom kutoka na kwenda katika starehe na kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume(viagra) na kukaa kwenye kumbi za starehe usiku kucha ,imemkera.

“Huyu akirudia nitajua kitu cha kumfanya,nimechoka kwa vile mara nyingi nimemvumilia lakini hasikii,nitamuonesha nini,kwa sasa sisemi,” alisema.

Lakini habari zaidi,zimeeleza kwamba mrembo huyo,amepanga kudai talaka endapo atagundua mumewe amerudia kutumia dawa hizo.

Hivi karibuni Odom, alitumia dawa hizo na kusababisha kuumwa na kulazwa hospitali ambapo alikuwa ana hali mbaya.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.