Lady Gaga apigwa kibuti

BURUDANI - - MBELE - NEW YORK, Marekani

MWANAMUZIKI na mwigizaji mashuhuri kutoka Marekani Lady Gaga amefichua kwamba yeye na mchumba wake wameachana.

Lady Gaga amewaomba mashabiki wawasaidie na kuwaunga mkono.

Msanii huyo na mchumba wake, Taylor Kinney, wamekuwa pamoja miaka mitano lakini uvumi umekuwa ukienea kuwa urafiki wao umekufa.

Amesema bado wanapendana sana lakini juhudi za kutaka kutimiza ndoto zao maishani, kuwa mbali pamoja na shughuli nyingi za kikazi vimetibua uhusiano wao.

Lady Gaga ambaye ana umri wa miaka 30, alichumbiwa na Kinney, ambaye ni mwigizaji na mwanamitindo, baada ya kukutana naye akiandaa video ya wimbo wa ‘ You and I’ mwaka 2011.

Alimchumbia Siku ya Wapendanao mwaka 2015, na akamvisha pete ya almasi ya umbo la moyo.

Wawili hao hawajapigwa picha sana wakiwa pamoja siku za karibuni.

Gaga, ambaye jina lake halisi ni Stefani Joanne Angelina Germanotta, pia ameonekana mara kadha akiwa hajavaa pete hiyo ya uchumba.

Mashabiki wao huwaita wawili hao ‘ Tayga’, kutokana na majina yao Taylor na Gaga.

Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakijiuliza hatima ya mbwa wanaomilikiwa na wapenzi hao, ambao majina yao ni Koji na Miss Asia Kinney.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.