‘Ndugu’ wa Ngoma atua Azam FC

BURUDANI - - MBELE - NA MWANDISHI WETU

NYOTA wa kimataifa wa Zimbabwe ambako pia anatoka staa wa Yanga Donald Ngoma, Bruce Kangwa, ametua nchini kufanya majaribio ya kujiunga na klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC.

Ofisa Habari wa timu hiyo, Jaffar Idd, alisema Kangwa anatokea timu ya Highlanders FC ya Zimbabwe inayoshiriki ligi kuu nchini humo.

Idd alisema Mzimbabwe huyo ameshacheza katika timu yake ya taifa mechi 20 na mpaka sasa yupo kwenye kikosi hicho.

Alisema anamudu kucheza nafasi tatu tofauti uwanjani, beki wa kushoto, winga wa kushoto na mshambuliaji.

Kangwa, anaungana na wachezaji waliokuwa kwenye majaribio ndani ya timu hiyo wakiwemo beki Mohamed Chicoto, Mossi Moussa Issa (wote Niger), mshambuliaji Ibrahima Fofana (Ivory Coast) na Fuadi Ndayisenga (Burundi).

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.