Tuzo imenifunza -Juma Abdul

BURUDANI - - HABARI -

BEKI wa Yanga, Juma Abdul, amesema kuwa amejifunza kitu baada ya kupewa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, msimu wa 2015/2016.

Akizungumza juzi, alisema kitendo cha kupewa tuzo hiyo, kimempa nafasi ya kufahamu kuwa ana kazi kubwa ya kuongeza bidii msimu ujao.

Alisema, amegundua bila ya kuzingatia nidhamu, bidii ya mazoezi na kusikiliza mafunzo ya makocha hawezi kutimiza lengo lake la kutaka kucheza soka ya kulipwa.

“Mimi bado nina imani ya kwenda kucheza nje, lakini kazi hiyo itatimia endapo nitaongeza bidii katika mazoezi ili niweze kucheza katika kiwango cha juu,”alisema.

Kauli hiyo, imekuja siku chache baada ya mwishoni mwa wiki, katika sherehe za utoaji wa tuzo hizo kwenye ukumbi wa Double Tree Hotel By Hilton, Masaki, Dar es Salaam,alitangazwa mshindi.

Abdul ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars amewashinda beki mwenzake, Mohammed Hussein ëTshabalalaí wa Simba na kiungo wa Mtibwa Sugar, Shizza Kichuya.

Kufuatia ushindi huo, Abdul mbali alikabidhiwa taji hilo na mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, pia atazawadiwa fedha Sh Milioni 9.2.

Hata hivyo, mchezaji huyo alipobanwa kuzungumzia kama amewahi kufanya mawasiliano na timu yoyote ya nje, aligoma kuzungimzia jambo hilo kwa undani zaidi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.