Mwigulu azipa shavu timu za Majeshi

BURUDANI - - HABARI -

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, amesema ana imani timu za majeshi zitarejesha makali yake msimu ujao wa Ligi Kuu.

Mwigulu akizungumza hivi karibuni na baadhi ya vyombo vya habari, alisema imani hiyo inatokana na kuwepo jitihada za ziada kuhakikisha timu hizo zinafanya vizuri.

Alisema, kuwepo kwa timu kama JKT Ruvu na Prisons ambayo imeshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi iliyopita na Ruvu Shooting ambayo imerejea Ligi Kuu kwa kishindo ana imani msimu ujao zitafanya vizuri na kutwaa ubingwa.

“Najua wameona kasoro zao, hivi sasa wanajiandaa watafanya vizuri ili kurejesha heshima,”alisema waziri huyo.

Hata hivyo, waziri huyo, amekiri kwamba imani hiyo inatokana na kuwepo nidhamu ya hali ya juu kwa wachezaji wanaounda timu hizo huku wakiwasikiliza kwa umakini makocha wao.

Aliongeza hata timu za Ligi Daraja la Kwanza, kutoka kwenye majeshi mbalimbali, zitaweza kufanya vizuri kutokana na kujipanga vyema kwa ajili ya msimu ujao wa ligi hiyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.