Kipre anauzwa Oman- Azam

BURUDANI - - HABARI -

MAKAMU Mwenyekiti wa timu ya Azam FC, Idrisa Nasssor, ameamua kuweka wazi kwamba wapo mbioni kumuuza mshambuliaji wa Kipre Tchetche kwa timu moja ya Oman.

Akizungumza juzi na baadhi ya vyombo vya habari, kiongozi huyo, alisema wapo kwenye mazungumzo ya mwisho.

Alisema timu hiyo inataka kumwaga fedha nyingi kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji huyo kutoka nchini Ivory Coast.

“Huyu hauzwi hapa nchini, mimi ni kiongozi wa juu wa Azam, nataka niweke wazi hakuna timu ya Tanzania ambayo imeonyesha nia ya kumpandia dau Kipre,kwa vile bado ana mkataba wa mwaka mzima na Azam,”alisema Makamu huyo.

Hata hivyo, kiongozi huyo alisema kama kuna timu ina nia ya kutaka kumsajili mchezaji basi milango iko wazi kwa ajili ya mazungumzo na wakifika bei wanayotaka wao wataweza kumuuza mkali huyo.

Kauli hiyo, imekuja baada yak uwepo tetesi kuwa mkali huyo anawindwa na timu za Simba na Yanga ili kumsajili kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu.

Hadi sasa, mchezaji huyo ameshindwa kuja Tanzania kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ana matatizo kwao Ivory Coast kuhusu kutapeliwa nyumba baada ya kununua.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.