Mwadui yamtema Nizar Khalfan

BURUDANI - - HABARI -

UONGOZI wa timu ya Mwadui FC ya Shinyanga, umetangaza kuwatema wachezaji 10 akiwemo nyota Nizar Khalfan.

Katibu Mkuu wa timu hiyo, Ramadhan Kilao , alisema jana kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya kupitia baadhi ya vigezo.

Alisema mbali na Nizar wengine waliotemwa ni Jabir Aziz ëStimaí, Bakari Kigodeko na Razack Khalfan. Nizar na Razack ni ndugu. Wengine ni Jamal Mnyate ambaye ametua Simba, David Luhende, Anthony Matogolo, Athuman Idd ‘ Chuji’ na wengine wawili ambao alishindwa kuwataja.

Aliongeza kuwa nafasi za wachezaji hao zitazibwa na wachezaji wengine sita ambao wamepanga kuwasajili.

“Kweli hao ni baadhi ya wachezaji ambao tumewaacha, mwingine amekwenda kufanya majaribio TP Mazembe,”alisema.

Katibu huyo, alisema kikosi chao kinatarajiwa kuanza rasmi mazoezi Jumatatu ijayo kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya ligi kuu msimu ujao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.