Wanandoa waahidi dhahabu Australia

BURUDANI - - KIMATAIFA -

SYDNEY, AUSTRALIA

WANAMICHEZO wanandoa kutoka Australia, Charlotte Caslick na mumewe Lewis Holland, wamesema watahakikisha wanapeperusha vyema bendera ya nchi yao na kutwaa medali za dhahabu katika michezo ya Olimpiki.

Wanandoa hao kutoka Magharibi wa jiji la Sydney kwa pamoja wataiwakilisha nchi yao kupitia mchezo wa rugby.

Nyota hao ambao wapo katika kikosi cha kwanza cha timu za mchezo huo, ni miongoni mwa wanamichezo wanaotarajiwa kuipatia Auastralia medali za dhahabu.

Akifanya mahojiano na jarida la The Daily Telegraph, Charlotte alisema ni matarajio yake kuwa atafanikisha malengo yake kupitia michezo hiyo na kupeperusha vyema bendera ya nchi yake.

“Ni raha kuona kuwa mimi na mwenza wangu tunakwenda katika michezo huku tukiwa na matumaini ya kufanya vyema na kurudi nyumbani tukiwa na medali,” alisema Charlotte.

Licha ya kucheza Rugby, Charlotte pia ni mwanamitindo ambaye anasema amejaribu kujikita zaidi katika mitindo lakini ameona mchezo wa rugby ndio kila kitu kwake.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.