Aing’ang’ania jezi namba 7

BURUDANI - - AFRIKA -

MCHEZAJI mpya wa Chelsea, N’Golo Kante amesema anapenda kutumia jezi namba 7 mgongoni ili kuhakikisha anaonyesha kiwango kwa kushirikiana vyema na wachezaji wenzake kuipa matokeo mazuri timu hiyo.

Akizungumza jana na baadhi ya vyombo vya habari, mchezaji huyo amesema kuwa amefurahi kujiunga na timu hiyo kwa ajili ya kuichezea msimu ujao katika mashindano mbalimbali ikiwemo Ligi Kuu ya nchini humo.

Mkali huyo amesajiliwa na Chelsea hivi karibuni kwa dau la paundi milioni 32, akitokea Leicester City ambapo alisema anapenda kutumia jezi yenye namba hiyo ili kuweza kutimiza lengo la kufanya vizuri katika michuano yote inayowakabili.

Kante yupo katika mapumziko hivi sasa, anatarajiwa kujiunga na kikosi cha Chelsea wiki hii kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya utakaoanza mwezi ujao ambapo timu hiyo, imeweka kambi yake nchini Marekani.

Nyota huyo, amechukua namba ya kiungo Mbrazil, Ramires Santos, ambaye aliondoka katika timu hiyo, Januari, mwaka huu na kujiunga na timu ya Jiangsu Suning.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.