Sitaki vitambi -Guardiola

BURUDANI - - MBELE - MANCHESTER, England

KOCHA Mkuu wa timu ya Manchester City, Pep Guardiola, amesema ana kazi kubwa ya kupunguza uzito wa mastaa wa timu hiyo ili waweze kucheza vizuri katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Uingereza na michuano mingine ambayo itawakabili.

Guardiola amelieleza gazeti moja la nchini humo kuwa, amegundua baadhi ya wachezaji wa timu yake wameongezeka uzito kitu ambacho kimeathiri uwezo wao wa kucheza soka.

Alisema kitendo cha wachezaji hao kuongezeka uzito kimeweza kupunguza nguvu,kasi ya kukimbia jambo ambalo limeanza kumpa ugumu wa kazi yake.

Miongoni mwa wachezaji ambao wameonekana kuongezeka uzito na kumshutua kocha huyo mpya wa Man City ni Samir Nasri.

Nyota mwingine ambaye ametakiwa na kocha huyo kupungua uzito ni Gael Clichy, ambapo kocha huyo amekuwa akiwa mazoezi tofauti na wenzao.

Pia kocha huyo, amekuwa anafuatilia chakula ambacho wanatumia wachezaji wake, ili kujua kinakwenda sambamba na mazoezi ambayo anawapa huku akiwataka kubadili tabia zao na kuweka mbele nidhamu ya mchezo wa soka tofauti na msimu uliopita.

Guardiola , amependekeza wachezaji wa timu hiyo wasizidi uzito zaidi ya kati ya kilo 60 hadi 70, amesema zaidi ya hapo wachezaji wanakuwa katika hatari ya kuumia kila mara na kusababisha matatizo kwenye timu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.