MO kuigawa Simba

BURUDANI - - MBELE -

BAADHI ya wachezaji wa zamani wa timu ya Simba, wameonekana kugawanyika kama klabu hiyo itampa hisa asilimia 51, Mohamed Dewji au vinginevyo.

Hatua hiyo, imekuja baada ya nyota wa zamani wa timu hiyo kwa nyakati tofauti, Omary Gumbo na Zamoyoni Mogella kutoa maoni yao.

Wachezaji hao walionekana kugawanyika huku kila mmoja akitoa maoni yake kuhusu hatima ya klabu hiyo kuelekea kwenye mkutano mkuu wa wanachama wa klabu hiyo.

Mkutano huo, umepangwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii Jijini Dar es Salaam ambapo Gombo alisema ni vyema mfumo wa kuuza hizo ukaangaliwa kwa umakini mkubwa.

Gumbo ambaye amewahi kuichezea timu hiyo na kuwa Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, alisema ni mapema mno kufanya hivyo.

Aliongeza kuwa ni vyema kufahamu anapewa kama nani au mfumo upi ambao utaweza kumpa nafasi Dewji kununua hizo na kubakisha nyingine 49 kwa klabu.

Alisema lengo ni kuweka taratibu kujua klabu itanufaika kivipi endapo wanachama watakubaliana juu ya jambo hilo huku wanachama nao wakiwa na mchango wao ndani ya klabu hiyo.

Lakini Zamoyoni Mogella amesema yeye anaona mfumo wa mabadiliko ndani ya klabu hiyo umechelewa kufanyika kwa vile hivi sasa soka inabadilika kila kukicha.

“Mimi naona soka imebadilika , vyema mfumo ukabadilika na kuwepo mfumo wa hizo hisa ili klabu iweze kufanya vyema katika mashindano mbalimbali,”alisema.

Akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari, Mohamed Dewji alisema tayari wapo kwenye mazungumzo na rais wa klabu hiyo, Evance Aveva ili kukamilisha mpango huo.

ìUnajua kila mtu ana interest, hakuna interest ya klabu, mimi nimeona sitaki nijihusishe na klabu ambayo haitafanikiwa, ndio maana mimi nilikuwa nasema Azam itakuja kufanya vizuri zaidi kuliko Simba na Yanga na wameanza,î alisema.

ìNimeongea na rais wa Simba na ameniambia nimwandikie paper. Unajua mimi nimemwambia ëwewe unafikiria mimi nikinunua hisa 51% ya Simba, maana yake nitaipeleka wapi? Mimi ni mtu wa hapa hapa na naipenda Simba. Leo mashabiki wa Manchester United, Arsenal they donít care klabu ya nani, wanachohitaji ni mafanikio. Mimi nimewaambia nipo tayari niwekeze bilioni 20. Leo Katumbi wa TP Mazembe ni timu yake na inafanya vizuri. Mimi nimewaambia hata nikiwekeza bilioni 20 sitaona hela, mimi na biashara mia nyingine ninapata hela,” alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.