Zidane amgeuzia kibao Pogba

BURUDANI - - MBELE - CALIFORNIA, Marekani

KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane, ametoboa siri bado ana mpango wa kutaka kumsajili nyota wa Juventus ya Italia, Paul Pogba kwa ajili ya kuichezea timu hiyo msimu ujao katika mashindano mbalimbali. Akizungumza jana na baadhi ya vyombo vya habari nchini Marekani, alisema bado yupo kwenye mikakati ya kumsajili mchezaji huyo kwa vile ana imani ataweza kutoa mchango mkubwa katika kikosi chake ili kiweze kufanya vizuri.

Alisema anastahili kujiunga na Real Madrid na ana nafasi kubwa ya kupata mafanikio kwa vile klabu hiyo ni kubwa , alisema tofauti na timu nyingine ingawa hakuwa tayari kueleza kwa undani zaidi juu ya mpango huo.

Madrid imepanga kumsajili mchezaji huyo ambaye anatakiwa pia na timu ya Manchester United, ambayo imeonyesha nia ya kutaka kumsajili huyo kwa gharama ya dau la Euro milioni 110 ambapo hadi sasa mazungumzo ya kutua United yanaendelea.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.