Simba wamejipanga

BURUDANI - - HABARI - NA NASRA KITANA

KAMATI ya Mipango ya klabu ya Simba imeanza mchakato wa kusaka dawa ya kuisaidia timu hiyo msimu ujao kuwa na mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara.

Kamati hiyo iliteuliwa hivi karibuni na Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva, inaundwa na wajumbe wanne ambao ni Ally Sulu, Aziz Kifile, Mulamu Ng’hambi na Seleman Omari.

Aveva aliiteua kamati hiyo kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo katika misimu minne iliyopita.

Ng’hambi, ambaye ni mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, alisema jana kuwa tayari kamati yao ishakutana na kuanza kazi kama iliagizwa na Aveva.

Alisema kamati hiyo itaangalia maeneo mbalimbali ambayo yakiwa sawa Simba itapiga hatua zaidi, hivyo watafanya mchakato huo kwa kuwashirikisha watu mbalimbali ndani ya timu na nje.

“Tutazungumza na makundi hayo, tuna imani kuna kitu tutakipata, na hata Dewji (Mohamed) tutazungumza naye, kwani maoni yake pia yatatufanya kufikia kile tunachokikusudia,”alisema Ng’hambi.

Aliongeza kuwa, wana imani mara baada ya kuzungumza nao, watajua nini sababu na hapo ndipo watatafuta dawa ya kumaliza tatizo hilo na Simba itapiga hatua zaidi hasa kuanzia msimu ujao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.