Hatutishwi na yeyote-Azam FC

BURUDANI - - HABARI -

UONGOZI wa timu ya Azam FC, umeeleza kwamba kamwe hautishwi na timu yoyote kutokana na kuwepo kwa usajili wa wachezaji wenye majina makubwa kwa sababu mpira unachezwa dimbani.

Kauli hiyo, imetolewa juzi na Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Nassor Idrisa wakati akizungumza na Burudani Jijini Dar es Salaam.

Amesema wao wananendelea kujianda ili kusuka kikosi chao kiweze kutetea ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati, kisha kusaka ubingwa wa Ligi Kuu.

Alisema wao wanafanya kazi kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi na si kuangalia wachezaji wenye majina makubwa ambao wakati mwingine wamekuwa hawana faida yoyote kwenye timu hiyo.

“Sisi hatuogopi timu yoyote,tunasuka kikosi chetu tumeanza na benchi la ufundi baada ya kuja makocha kutoka Hispania, tunamazilia kwenye kikosi kwa kusajili wachezaji walio na msaada,”alisema kiongozi huyo.

Makamu huyo, alitamba kuwa, kamwe Azam FC haiogopi timu yoyote kwa vile kikosi chao kipo vizuri kuliko timu nyingine na kina uwezo mkubwa wa kuivua ubingwa wa Ligi Kuu timu ya Yanga katika michuano hiyo ya msimu ujao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.