JKT Ruvu wajigamba

BURUDANI - - HABARI -

KOCHA Mpya wa timu ya JKT Ruvu, Malale Hamsini, amesema ana imani msimu ujao kikosi chake kitaonyesha uwezo mkubwa baada ya kufanyika usajili wa makini chini ya Mkurugenzi wao wa ufundi, Abdallah Kibaden.

Akizungumza jana, alisema kuwepo kwa Kibaden ndani ya kikosi hicho kimeweza kusaka wachezaji ambao wana uwezo mkubwa wa kucheza soka hasa vijana ambao amekiri damu yao bado inachemka sana.

Alisema pamoja na yeye kuingia ndani ya kikosi hicho hivi karibuni, bado ana imani kwamba kazi ya kusaka ubingwa msimu ujao, itakuwa nzuri kwao kutokana na kuwepo benchi zuri la ufundi na wachezaji wenye kufahamu nini wanatakiwa kufanya.

“Tupo makini, tumeanza kazi kwa kuangalia uwezo wa kila mchezaji, lengo kufahamu mapema wapi kuna kasoro, nina imani msimu ujao, tutafanya vizuri na kushika nafasi za juu ikiwemo kutwaa ubingwa wa bara,”alijigamba kocha huyo mpya.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.