Mbeya City kamili ligi kuu

BURUDANI - - HABARI -

KIKUNDI cha burudani kutoka Geita, kikitoa burudani wakati wa uzinduzi wa shindano la Shinda Gari ambalo lilizinduliwa juzi Mkoani Geita. Shindano hilo litafanyika mikoa 13 nchini na magari 25 yatashindaniwa.(Na Mpigapicha Wetu) UONGOZI wa klabu ya Mbeya City umesema timu yake haina mpango wa kucheza tena mchezo wowote wa kujipima nguvu kabla ya kuanza ligi hiyo.

Ligi hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 20 mwaka huu katika viwanja mbalimbali ikishirikisha timu 16.

Ofisa Habari wa Mbeya City, Dismas Ten, alisema timu yake haitacheza michezo hiyo ili kutoa nafasi kwa wachezaji kupumzika na kufanya mazoezi mepesi kabla ya kuanza mashindano.

Ten alisema timu yake imeimarika na ipo tayari kwa michuano hivyo ni vyema wachezaji wakapumzika ili kuepeka majeruhi pindi watakapocheza michezo mingine ya kirafiki.

Alisema kabla ya hapo uongozi ulipanga kuipeleka timu nchini Malawi kucheza mechi za kirafiki lakini waliamua kufuta safari hiyo baada ya ratiba kuvurugika.

“Kwa sasa wachezaji wanaendelea na mazoezi na wote wapo katika hali nzuri na ninaamini kuwa tutaanza ligi kwa kufanya vyema baada ya kufanya maandalizi ya kutosha,” alisema Ten.

Alisema licha ya kujiandaa vyema, benchi la ufundi limefanya usajili ambao utakuwa na manufaa makubwa msimu ujao.

Aliongeza kwa kusema usajili huo utakifanmya kikosi chake kuwa moto wa kuotea mbali na kujijengea heshima tangu mwanzo wa msimu hadi mwisho. TIMU ya Azam FC leo inashuka dimbani kuivaa timu ya Mamlaka ya Mapato Uganda (URA), katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.

Mechi hiyo ni maalumu kwa Azam ambayo inajiwinda na michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayoanza kutimua vumbi Agosti 20 mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam, jana, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Jaffar Idd, alisema maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yamekamilika na kikosi chake jana kilifanya mazoezi mepesi tayari kwa mchezo huo.

Idd alisema benchi la ufundi la timu yake litatumia mchezo huo kuangalia uwezo wa wachezaji wake ikiwa ni pamoja na kurekebisha kasoro ndogondogo kabla ya kuanza kwa ligi.

“Timu yangu ipo vizuri na wachezaji wote wana afya njema na hadi jana jioni hatukuwa na majeruhi yeyote hivyo nina imani kuwa mchezo wa leo utakuwa mzuri na timu yangu itaibuka na ushindi,” alisema Idd.

Alisema hadi sasa timu yake imekwishacheza michezo miwili ya ndani ya kirafiki dhidi ya JKT Ruvu na Ruvu Shooting zote za mkoa wa Pwani.

“Nawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi waje waishangilie timu yao na waone jinsi ilivyoandaliwa kabla ya kuanza kwa ligi,” aliongeza Idd.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.