Yanga kukodishwa, mabadiliko Simba

BURUDANI - - MBELE -

NA MWANDISHI WETU YANGA na Simba ni klabu zinazoweza kuitwa kulwa na doto kutokana na kufanana mambo mengi.

Kwa kawaida, Simba ukitokea mgogoro upande wa Yanga unakuwa shwari. Si kwamba utulivu huo huchukua miaka mingi la asha! Miezi au mwaka mmoja baadaye bundi huhamia Jangwani pia. Imetokea hivyo mara nyingi.

Mifano kuhusu mienendo ya klabu hizi ni mingi, lakini ulio hai kabisa wa hivi karibuni ambao unatokana na klabu hizo kutaka kuingia katika mfumo wa kuuza hisa. Imeanza Simba sasa zamu ya Yanga.

Zinajiandaa kuhama kwenye mfumo wa klabu za wanachama na kuwa kampuni ambazo zitauza hisa na ‘mwenye kisu kikali’ ndiye atakula nyama.

Ni mipango mizuri sana kwa maslahi ya soka la Tanzania kwa kuwa dunia ya maendeleo inahitaji hivyo.

Mpira siku hizi sio mdomo mtupu, soka linahitaji uwezekezaji mpana na ndipo mafanikio hupatikana kama inavyokuwa kwa klabu mbalimbali duniani.

Mathalani siku tatu zilizopita klabu ya Manchester United ilivunja benki na kulipa pauni milioni 105 ambazo si pesa za kitoto kumrejesha katika klabu hiyo kiungo Paul Pogba kutoka Juventus ya Italia.

Je, kwanini Manchester United imefanya hivyo? Kwa sababu kocha Jose Mourinho anajua mchezaji huyo ataleta matunda klabuni hapo.

Mosi, klabu itapata pesa nyingi kwa kuuza kama njugu jezi za Pogba pili, Mfaransa huyo atatoa mchango stahiki uwanjani na kupandisha thamani ya klabu.

Pia Manchester United imefika hatua ya kufanya Pogba na wengine wawe wachezaji ghali duniani kwa sababu klabu inaendeshwa kibiashara na wanaofanya kazi hiyo ya usimamizi ni wataalamu haswa pale ‘O.T’.

Swali la kujiuliza. Manchester United, Arsenal, Real Madrid au Bayern Munich ziligeuzwa kuwa za kibiashara kwa njia ya ujanja ujanja? Jibu lake hapana na kama kungekuwa na usanii wowote leo hii zingekuwa ‘zimeaga dunia’ kabisa!

Isingekuwa rahisi Manchester United yenye karne zaidi ya moja kuwepo mpaka sasa kwani kama ingeingizwa katika mageuzi kwa ajili ya kulenga kuwanufaisha waliotoa mawazo tu, sasa hivi timu hiyo isingekuwepo ama nyingine zinazovuma wakati huu.

Zingegeuka kifo cha mende kwa sababu ya kuingia katika mabadiliko kwa njia za vificho, na hilo ndio jambo linalopaswa kutazamwa na klabu za Simba na Yanga zilizoamka sasa kutoka kwenye usingizi wa pono.

Kabla ya kwenda katika mabadiliko hayo, kuna maswali 10 ambayo viongozi wa Simba na Yanga na wanachama wao wanatakiwa kujiuliza:

Kwanini Mwenyekiti wa Yanga Yussuf Manji anataka kukodi nembo na timu ya Yanga kwa asilimia 75 zake, na 25 ziwe za klabu? Pia, kwa sababu zipi mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’ amesema auziwe hisa asilimia 51 na Simba zibaki asilimia 49 kwa sh bilioni 20?

Hakuna uwazi hasa kwa nini Manji amepanga kuikodi timu ya Yanga na nembo badala angewasilisha ombi la kufanya hivyo na kusubiri apangiwe kiasi anachotakiwa kulipa.

Si sahihi Manji kusema anataka asilimia 75 wakati hakuna anayejua thamani ya ‘Yanga majengo na uwanja wa Kaunda’ ni asilimia 25 ambazo sawa na shilingi ngapi baada ya kukokotolewa?

Swali hili linamgusa pia ‘Mo’, Simba ina asilimia 49 kwanini sio 51 hadi 60?

Manji na Mo wana haraka gani mpaka wanataka kuwekeza kwa kutangaza mabadiliko au ukodishaji ukamilishwe ndani ya muda mfupi?

Hakuna uhalali wa kufanya haraka kwenye mabadiliko makubwa kama haya. Simba na Yanga si klabu za kuendeshwa kwa pupa kutokana na historia yake katika nchi hii na siku zote haraka haina baraka.

Wanachama na viongozi wanapaswa kueleweshwa nini maana ya kukodisha au kununua hisa kisha ifanyike michakato hiyo kufuatana na maridhiano na sio bora makubaliano.

Kuzivuruga Yanga na Simba sawa na kuyumbisha mustakabali wa taifa inafahamika klabu hizi zimeshiriki kwa namna moja au nyingine kutafuta uhuru wa nchi, kujenga mshikamano, kudumisha amani na kuleta upendo miongoni mwa jamii. Wafuasi wake wanazidi milioni 20 ambao ni nusu ya Watanzania.

Nani atamuhoji Manji kuhusu mapato ya klabu wakati yeye ndio mwenyekiti na wakati huo huo mmiliki wa Kampuni ya Quality Group? Kiongozi gani wa Simba anaweza kusimama hadharani kupinga wazo la Mo hasa wakati huu wa vuguvugu la kutaka mabadiliko?

Anachofanya Manji katika Yanga kina mgongano wa maslahi kutokana na yeye kuwa mwenyekiti wa klabu ambayo itapaswa ailipe asilimia 25 ya faida kama anavyotaka, lakini nani wa chini yake atathubutu kusema klabu inanyonywa?

Pia, Mo ametumia kigezo kipi kutangaza anunue hisa asilimia 51 za Simba kwa thamani ya sh bilioni 20. Kwa akili ya kawaida, Simba inaweza kuuza hisa na kuvuna zaidi ya sh bilioni 100 nini bilioni 20 alizojipangia Mo!

Kwa kuwa mfanyabiashara huyo anajua pesa alizotangaza kwa wana Simba ni nyingi na hasa kwa kuzingatia wamechoka kuitwa wa mchangani kutokana na kufanya vibaya misimu minne, zinatosha kuwa chambo cha kuwashawishi

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.