Zilizobamba

MWIGIZAJI wa filamu nchini Jennifer Kyaka ‘Odama’ ametupia katika ukurasa wa Facebook, picha yake inayoonyesha ana furaha na kuandika “Furaha ya kweli maishani

BURUDANI - - MBELE - Na Nasra Kitana 0717 366 789

BAADA ya mashabiki kumsimanga kuwa anamuiga bosi wake, Nassib Abdul ‘Diamond’, msanii Rajabu Abdulkharim ‘Harmonize’, amejibu shutuma hizo kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram: “Nina imani nitafika kwa uwezo wa alie juu kwani yeye ndio kila kitu”.

MWIGIZAJI wa filamu nchini Jennifer Kyaka ‘Odama’ ametupia katika ukurasa wa Facebook, picha yake inayoonyesha ana furaha na kuandika “Furaha ya kweli maishani hailetwi na mtu bali na wewe mwenyewe, ishi ukimtumainia Mungu na kamwe hatokuacha, God is great.”

MWANAMITINDO Jokate Mwegelo ‘ Kidoti’ ameeleza anapenda amani kama ambavyo amefafanua kupitia akaunti yake ya Instagram. “Naipenda amani sipendi ugomvi.”

WACHEZAJI soka mbalimbali wamempa pole kipa wa timu ya Yanga, Deogratius Munish ‘Dida’ kwa kufiwa na baba yake mzazi mwishoni mwa wiki iliyopita.

Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta, Simon Msuva na Aishi Manula ni miongoni mwa wachezaji waliotoa pole hiyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.