Kumekucha Simba

BURUDANI - - HABARI -

KOCHA Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, ametoboa siri kama wapo mbioni kubadili mfumo wa kushambulia katika kikosi chao, ili waweze kupata mabao zaidi kwenye michuano ya msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na Burudani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam alisema lengo la kufanya hivyo ni kutaka kuhakikisha wanatoa dozi kwa timu zote, ambazo watapambana nazo huku wakijenga mfumo mzuri wa kujilinda.

Alisema kazi hiyo, wameanza kuifanya na ndio maana kuna wakati wanaweka baadhi ya wachezaji nje wakati wa mechi, ili waweze kusoma mbinu za wapinzani wao kabla ya kuwaingia hasa kipindi cha pili kufanya kazi hiyo.

“Unajua soka ni mchezo wa kusoma nini mwenzako anakifanya. hapo unaweza kupata jibu nawe ufanye nini ili uweze kupata ushindi. Kuna wakati inabidi tufanye kazi ya kuwaweka nje baadhi ya wachezaji wenye viwango vikubwa, ili wasome mchezo na kisha tunawapa maelekezo ambayo wakiingia yanakuwa na faida kwa timu yetu,”alisema.

Kauli hiyo, imekuja baada ya baadhi ya washabiki wa timu hiyo kushangaa kitendo cha benchi la ufundi, linaloongozwa na kocha wao, Joseph Omog kumweka nje Ibrahim Ajib, ambaye anaanika kuwa na kiwango bora katika mchezo dhidi ya JKT Ruvu, uliochezwa wiki iliyopita ambapo uwanjani kipindi cha pili.

Kwenye mchezo huo, timu hizo zilitoka suluhu na kugawana pointi moja kila mmoja katika mchezo wa ligi hiyo, ambao ulikuwa na ushindani mkubwa muda wote wakati unachezwa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.