Waziri anunua kila bao la Mbao FC

BURUDANI - - HABARI -

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amesema atatoa sh. 50,000 kwa kila bao, ambalo wachezaji wa Mbao FC watafunga kwenye kila mechi ya msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Angelina ambaye ni Mbunge wa Ilemela (CCM), mkoani Mwanza alisema hayo wakati akizungumza na wachezaji wa timu hiyo kuwa amepanga kufanya hivyo ili kuwapa hamasa wachezaji wa timu hiyo wanaotoka katika jimbo lake.

Alisema anajisikia faraja kubwa kuona wilaya hiyo ina timu, ambayo inashiriki michuanio hiyo mikubwa hapa nchini na kueleza kwamba ana imani wachezaji wa timu hiyo watachangamkia ofa hiyo.

“Najua tumeteleza katika mchezo dhidi ya Mwadui kwa kufungwa bao 1-0, tusikate tamaa ligi bado mbichi na nina imani michezo ijayo mtashinda. Kila bao nitawapa sh. 50,000, jitahidini bado tuna nafasi ya kufanya vizuri,”alisema.

Mchezo huo ni wa pili kwenye ligi hiyo, baada ya awali kucheza na Stand United ambapo zilitoka suluhu katika mechi iliyofanyika kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.