Wachezaji Mbeya City bado - Phiri

BURUDANI - - HABARI -

KOCHA Mkuu wa timu ya Mbeya City, Kinnah Phiri, ametoboa siri kwamba kikosi chake bado hakijaimarika kutokana na ujio wa baadhi ya wachezaji wapya kwenye timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu msimu huu.

Phiri alieleza hayo wakati akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari mjini Mwanza, kama amegundua wachezaji wake wanapoteza nafasi nyingi za kufunga mabao kutokana na kutozoea mfumo wa uchezaji.

Alisema hayo hiyo, kufuatia kuwepo baadhi ya wachezaji wageni ndani ya kikosi chake kitu ambacho kimekuwa kinasababisha timu hiyo kutofanya vizuri, licha ya kushinda mchezo dhidi ya timu ya Toto African kwa bao 1-0.

Mchezo huo, ulifanyika kwenye dimba la CCM Kirumba, ambapo kocha huyo alisema, kama wachezaji wake wangetulia ana imani siku hiyo wangeweza kushinda kwa idadi kubwa ya mabao kwenye mchezo uliofanyika mwishoni mwa wiki.

“Nataka kuweka nguvu zaidi kwa washambuliaji wajue nini cha kufanya hasa wanapoingia katika eneo la hatari, kazi hiyo nitaifanya kabla ya kucheza na Mbao FC, lakini najua wapo baadhi ya wachezaji wageni hawajazoea mfumo wa uchezaji wa kikosi changu,”alisema kocha huyo kutoka nchini Malawi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.