Patric Liewig akalia kuti kavu Stand Utd

BURUDANI - - HABARI -

UONGOZI wa timu ya Stand United, umeanza kumchunguza kocha wao mkuu, Patrick Liewig, ili kujua uwezo wake wa kufundisha na ukaribu wake kwa wachezaji, baada ya kuonyesha kitendo cha utovu wa nidhamu.

Akizungumza jana, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Kennedy Nyangi, alisema wameanza kazi hiyo baada ya kocha huyo kutoka Ufaransa, kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu na huenda wakamchukulia hatua kali.

Alisema, hatua hiyo inatokana na kocha huyo kulumbana wazi wazi na msaidizi wake Athuman Bilal, kitu ambacho wameona wakifanyie kazi na huenda wakagundua mambo mengi makubwa yanayochangia kufanya vibaya katika Ligi Kuu.

“Tunajaribu kumuangalia huyu kocha, tumegundua huenda ana matatizo na pengine yanachangia timu kupata matokeo mabaya, wakati wowote tutatoa ufafanuzi kuhusu mwenendo wake wa utovu wa nidhamu baada ya kutoa lugha chafu kwa viongozi wenzake wa benchi la ufundi na mambo mengi,” alisema Katibu huyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.