ZAMU YA SIMBA

BURUDANI - - MBELE - NA NASRA KITANA

MSHAMBULIAJI wa Simba, Laudit Mavugo (kulia), akimtoka beki wa Ruvu Shooting, Damas Makwaya, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, jana. Simba ilishinda mabao 2-1. (Picha na Jumanne Gude).

NI zamu ya Simba kushusha mikong’oto katika ligi kuu ya Tanzania bara baada ya jana kuwachezesha kwata Ruvu Shooting mabao 2- 1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Timu hiyo tayari imeshinda mbili za ligi kuu msimu huu na kutoka sare moja, hivyo ina pointi saba sawa na Mbeya City inayoendelea kukaa kileleni mwa msimamo kufuatia kuongoza kwa mabao ya kufunga.

Katika mechi ya jana, Simba ilipata mabao mawili yaliyofungwa dakika ya 11 na dakika ya 48 na Ibrahim Ajib na Laudit Mavugo na kuwazima Ruvu waliotamba wiki nzima kuwa wangetoka kifua mbele katika mchezo huo.

Timu hizo zilianza mche- zo zikishambuliana kwa zamu na Ruvu Shooting ilikuwa ya kwanza kufunga bao dakika ya nane kupitia Abrahman Mussa. Mfungaji aliwatoka mabeki wa Simba na kutumbukiza mpira wavuni.

Simba walikuja juu na kusawazisha bao hilo kisha kucheza kwa kasi huku ikikosa mabao mawili ya wazi dakika ya 19 na 23 kupitia kwa Mavugo.

Ruvu nayo ilijibu mashambulizi na dakika ya 38 Said Dilunga aliwatoka mabeki wa Simba na kubaki na kipa lakini mpira aliopiga ulitoka nje.

Simba ilizidi kuamka zaidi katika kipindi cha pili baada ya kufanya mabadiliko kwa kuwaingiza Jamal Mnyate, Mzamiru Yassin na Fredrick Blagnon. Lakini wachezaji wa Ruvu walizuia hatari zilizoelekezwa langoni mwao.

Katika mchezo huo, mwamuzi Ngole Mwangole wa Mbeya aliwaonya kwa kadi za njano Ajib, Blagnon na Novart Lufunga wa Simba, huku Jabir Aziz ‘Stima’ akionyeshwa kadi nyekundu na Issa Kanduru wote wa Ruvu Shooting kadi ya njano.

Kutokana na matokeo hayo, Simba imekwea hadi nafasi ya tatu ikiwa na pointi saba sawa na Mbeya City na Azam FC zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Baada ya mchezo huo, uongozi wa Simba ulitoa kitita cha sh. milioni 10 ‘live’ na kumpatia meneja wa timu hiyo, Mussa Hassan ‘Mgosi’ na kuwagawia wachezaji kama motisha ya ushindi.

Wakati Simba iking’ara, mahasimu wao Yanga walilazimishwa suluhu na Ndanda FC katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Mchezo mwingine uliikutanisha Azam FC na Prisons ya Mbeya katika Uwanja wa Sokoine na wana lambalamba walishinda 1-0.

Simba: Vicent Angban, Malika Ndeule, Mohamed Hussein, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Mnyate, Said Ndemla/Mzamiru Yassin, Laudit Mavugo/ Fredrick Blagnon, Ibrahim Hajib na Kazimoto. Ruvu Shooting: Abdallah Rashid, Damas Makwaya, Mau Bofu, Frank Msese/ Renatus Kisase, Shaibu Nayopa, Jabir Aziz, Abdulhaman Mussa, Shaban Kisiga, Said Dilunga, Fulgence Maganga na Claide Wigege.

Msimbazi 2-1 JKT

Ndanda 0-0 Yanga

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.