Neymar aibeba tena Brazil

Brazil 2, Colombia 1

BURUDANI - - MBELE -

BAO la pili la Neymar lilitosha kuipa Brazil ushindi wa 2-1 dhidi ya Colombia juzi katika hekaheka za kufuzu Kombe la Dunia nchini Russia 2018 na kuwawezesha mabingwa hao wa zamani wa dunia kutakata mechi ya pili mfululizo.

Wenyeji Brazil walianza mchezo vizuri baada ya sekunde 80 baada ya Miranda kuruka kichwa na kutupia wavuni mpira wa kona uliozaa bao la kwanza. Ilikuwa mechi ya 33 kwa mchezaji huyo katika timu ya taifa.

Brazil, ikicheza mechi yao ya pili chini ya kocha mpya Tite, ilitawala mchezo kipindi cha kwanza kwa kugonga pasi nyingi lakini walishindwa kutumia nafasi walizopata kufunga hatua iliyowagharimu kufuatia Colombia kusawazisha dakika 35.

Bao hilo lilikuwa la kujifunga baada ya James Rodriguez kupiga mpira wa adhabu umbali wa mita 38 na beki wa Brazil, Marquinhos aliusindikiza kwa kichwa mpira huo kimiani. BRAZIL’S RECORD SCORERS Neymar aliyepokea pasi ndani ya eneo la hatari dakika ya 73 alivuta hatua chache na kupiga mpira ambao ulijaa wavuni kupitia kona ya lango kutokana na kumshinda kipa David Ospina.

Lilikuwa bao lake la 48 katika mechi za kimataifa 72 alizocheza Neymar na kufikia rekodi ya Zico kwenye orodha ya wafungaji vinara wa Brazil wakati wote.

Brazil inaongoza kwa pointi 15 na ipo mbele ya Argentina kwa tofauti ya mabao, huku kikosi hicho cha Lionel Messi chenyewe kikilazimishwa sare 2-2 dhidi ya timu inayoshika mkia Venezuela.

Colombia inazidiwa alama 10 na nchi hizo katika kundi lao lenye timu 10 za Amerika Kusini.

REKODI YA WAFUNGAJI BRAZIL

1. Pele: 77 2. Ronaldo: 62 3. Romario: 55 4. Zico, Neymar: 48 6. Bebeto: 39 7. Rivaldo: 35 8. Jairzinho, Ronaldinho: 33 9. Ademir, Tostao: 32

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.