MANJI JEURI

Yanga wote wajazwa fedha

BURUDANI - - MBELE - NA NASRA KITANA

UKISIKIA kujibu mapigo ndio huku ambapo Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, amewamwagia fedha wachezaji wake ili wafanye vyema katika ligi kuu Tanzania Bara.

Manji amewapa wachezaji hao fedha ikiwa ni siku chache baada ya klabu ya Simba kuanzisha kampeni ya kuwapa sh. milioni tano wachezaji wake katika kila mchezo watakaoshinda.

Mwenyekiti huyo alikutana juzi na wachezaji hao na kufanya nao mazunguzmo ya saa nne kabla ya kutoa kitita cha fedha kwa kila mchezaji kisha safari ya kwenda Mtwara kucheza na Ndanda FC ikaanzia hapo.

Kwa mujibu wa habari kutoka kwa mmoja wa wachezaji wa timu hiyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema fedha walizolipwa ni malimbikizo ya motisha walizokuwa wanadai.

Fedha walizolipwa wachezaji hao za bonasi za ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2015/16, ubingwa wa kombe la FA na kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Nyota huyo alidai licha ya motisha, walilipwa mishahara waliyokuwa wanadai na kutakiwa kuhakikisha wanashinda mchezo dhidi ya Ndanda, lakini jana wametoka suluhu.

Katika kikao hicho, mwenyekiti huyo aliwasisitiza nyota wake kuhakikisha kuwa hawafanyi makosa na hasa katika michezo yote ya mzunguko wa kwanza.

“Kama ni fedha mimi nitatoa na nitahakikisha hamdai chochote hivyo jukumu lenu kuhakikisha mnafanya vyema,” alisema Manji.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.