Unaishi Ilala? Miss wako utamjua kesho

BURUDANI - - HABARI -

WAREMBO 15 kesho watapanda jukwaani kuwania taji la Miss Ilala 2016 katika ukumbi wa Hyatt Regency Kilimanjaro, Dar es Salaam.

Mratibu wa shindano hilo, Tickey Kitundu, alisema maandalizi kwa ajili ya shindano hilo yamekamilika na warembo wote wapo tayari kwa shindano.

Alisema mshindi katika shindano hilo atajinyakulia sh. 1,000,000 na luninga kutoka kampuni ya StarTimes.

Alisema mshindi wa pili atalamba sh. 700,000, mshindi wa tatu sh. 300,000 na wanne sh. 200,000 huku mshindi wa tano akijishindia sh. 150,000 na washiriki wengine wakifutwa jasho kwa sh. 50,000 kila mmoja.

Tickey aliongeza kwamba warembo watakaoshika nafasi tatu za juu watakata tiketi ya kushiriki fainali za Miss Tanzania zitakazofanyika baadae mwaka huu.

Mwanamuziki Rubby atawasindikiza washiriki hao kukatiza jukwaani kwa kutoa burudani safi.

Wachezaji wa Uganda wakipongezana baada ya kuifunga Comoro na kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika mwakani. Timu hiyo imesota miaka 38 hadi kufuzu kwenye michuano ya Afcon.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.