Mourinho v Guardiola

BURUDANI - - HABARI - LONDON, England

DUNIA ya wapenda soka itasimama dakika kwa sababu ya mechi ya Manchester United na Manchester City timu ambazo ni mahasimu katika ligi kuu ya England.

Kutakuwa na upinzani wa aina mbili; kwanza ni kocha Jose Mourinho na Pep Guardiola waliotokea kupapatuana vilivyo katika mpira wa miguu na kuleta mvuto hasa na pili, ushindani wa timu zenyewe.

Mechi hiyo itaanza saa 8: 30 mchana kwa saa za Afrika Mashariki, ambapo kumbukumbu zinaonyesha uhasama wa soka kati ya makocha hao ulipamba moto rasmi katika ligi ya Hispania ‘La Liga’.

Guardiola alipokuwa kocha Barcelona na Mourinho Real Madrid, timu zao ziliundwa na wachezaji nyota na kufanya mchezo kuwa kati yao kuwa mgumu.

Baada ya vuta nikuvute za Hispania makocha sasa wamekutana England na upinzani wao utaamka kuanzia kwenye dimba la Old Trafford ambalo lina uwezo wa kuingiza zaidi ya mashabiki 70,000. Man City watakuwa wageni wa Mashetani Wekundu.

WALIPAISHA JIJI LA MANCHESTER

Kwa sababu yao, jiji la Manchester limegeuka nyumbani kwa makocha hao wapinzani wanaosifika pia kwa ubora wa kazi na hata kulumbana kisa kandanda.

Mara ya kwanza Guardiola na Mourinho kukutana wakiwa makocha na kuzua upinzani ilikuwa katika mechi ya Barcelona na Inter Milan iliyokwisha 0-0 katika ligi ya mabingwa Ulaya ndani ya uwanja wa San Siro mwaka 2009.

Katika marudiano, timu hiyo ya Hispania 2-0 ilishinda 2-0 Nou Camp japo wenyeji walicheza bila ya Lionel Messi au Zlatan Ibrahimovic, lakini Xavi aliwasambaratisha vijana wa Mourinho.

Baada ya kichapo hicho Mourinho alitamba kuwa timu yake ilicheza vyema na kuitaka Barca katika mchezo mwingine. Hatimaye ombi hilo lilitimia walikutana katika nusu fainali ya michuano hiyo ya Ulaya na Inter ilishinda 3-1 San Siro na baada ya hapo upinzani ulianza kukolea.

KUMBE MARAFIKI WA ZAMANI

Mourinho na Guardiola waliwa- hi kufanya kazi pamoja Barca kati ya mwaka 1996-2000, wakati huo Mourinho alikuwa kocha na mwenzake mchezaji.

Upande wa mataji kulingana na takwimu, Mourinho ameshinda 22 na Guardiola 21. Pia kila mmoja ametwaa ubingwa wa ligi mara tatu.

Guardiola amenyakua La Liga nchini Hispania na Mourinho kwenye ligi kuu ya England, ambapo katika mara 11 walizokutana, Guardiola ameshinda tano, sare nne, Mourinho mbili.

Upinzani wao uliongezeka mwaka 2010 baada ya Mourinho kuwa kocha wa Real Madrid na kipondo cha kukumbukwa ambacho Mourinho alipewa na Guardiola katika El Clasico ya kwanza kati yao ni kunyonyolewa 5-0 na Barcelona!

Vita yao imehamia katika ligi kuu ya England na shughuli pevu itaanza keshokutwa na mwamuzi Mark Clatterburg ndiye atakata mzizi wa fitina katika mchezo huo unaokuwa na presha nyingi kila Man City na Man United zipokutana.

Katika mechi mbili za msimu uliopita Man City ililazwa 1-0 katika duru la kwanza na la pili.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.