Mlawa kuwakosa Azam

BURUDANI - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

MSHAMBULIAJI wa Mbeya City, Geoffrey Mlawa hatacheza mchezo wa Jumamosi dhidi ya Azam FC kufuatia majeraha aliyopata kwenye mechi na Toto Africans uliopigwa jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Habari wa Mbeya City, Dismas Ten iliyotolewa jana, jopo na madaktari wa timu hiyo limelithibitishia benchi la ufundi kuwa Mlawa hawezi kucheza dhidi ya wana lambalamba hao.

Aidha, ofisa huyo amesema baada ya mapumziko ya juzi yaliyotolwa na kocha Kinnah Phiri kufuatia safari ndefu ya saa nyingi kutoka Kanda ya Ziwa katika mechi na Toto, kikosi cha Mbeya City jana kilianza mazoezi rasmi kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Azam.

Ten alisema nyota wote 30 ikiwa ni pamoja na 25 waliokuwa nje ya jiji la Mbeya kwa takribani wiki tatu kwa ajili ya michezo ya mwanzo wa msimu, walijumuika kwenye mazoezi hayo uwanja wa Sokoine juzi.

ìTumeanza mazoezi leo (juzi), baada ya mapumziko, nyota wetu wote wapo ikiwa ni pamoja na wale ambao hawakusafiri na timu kwenda Mwanza na Shinyanga kwenye michezo mitatu ya Mwanzo wa msimu ambayo tuliikamilisha kwa kushinda miwili na suluhu moja,” alisema.

Alisema matokeo hayo yameongeza molari ya kikosi chao katika ligi kuu msimu huu na kutamba kuwa Mbeya City imejipanga kuvunja rekodi zote ambazo ilikuwa haijawahi kuzifikia tangu ilipopanda daraja misimu mitatu iliyopita.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.