Mbeya City yazifunika Simba, Yanga ligi kuu

BURUDANI - - HABARI - NA CATHERINE NACY

LIGI kuu Tanzania bara ilitimua vumbi wiki iliyopita kwa baadhi ya timu kutafuta pointi tatu muhimu, lakini Mbeya City rekodi yao ilikuwa nzuri sana.

Timu hizo zilishuka dimbani Septemba 3 na 4 ili kuhakikisha zinapata pointi tatu na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi.

Miongoni mwa timu ambazo zilishuka dimbani ni pamoja na Mbao FC waliocheza na Mbeya City katika uwanja wa CCM Kirumba, huku katika uwanja wa Kaitaba Kagera Sugar waliwakaribisha Mwadui ya Shinyanga.

Majimaji ya Songea walikuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar huku JKT Ruvu wakishuka katika uwanja wa nyumbani wakiwa wenyeji wa African Lyon.

Septemba 4 kulipigwa mch- ezo mmoja ambapo Stand United waliwakaribisha Toto Africans katika uwanja wa Kambarage na katika michezo hiyo, Mbeya City ilivunja rekodi kwa kushinda 4-1 dhidi ya Mbao kwani tangu kuanza msimu huu, hakuna timu iliyoshinda idadi ya mabao kama yao.

Mwadui ya walifungwa bao 1-0 na mambo yalikuwa magumu kwa Majimaji kwani walitandikwa mabao 2-1 na Mtibwa, JKT Ruvu walimaliza mchezo kwa kugawana pointi na African lyon baada ya kutoka sare 1-1.

Stand walitoka kifua mbele katika uwanja wao wa nyumbani kwa kuwafunga Toto Africans bao 1-0. Ligi hiyo iliendelea jana na rekodi nyingine zilitarajiwa kuandikwa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.