Sokoine wapigiwa saluti

BURUDANI - - HABARI - NA SOLOMON MWANSELE, MBEYA

UWANJA wa Sokoine umetajwa ni moja ya viwanja bora vya soka hapa nchini.

Hayo yamesemwa na msemaji wa timu ya Azam FC Jaffer Idd, ambaye ameupongeza uongozi wa Chama Cha Soka Mkoa wa Mbeya (MREFA), kwa kuutunza vizuri uwanja huo na kuwa tofauti na viwanja vingine vyenye hali mbaya na havistahiki kutumika ligi kuu.

Alisema juzi kuwa walifanya mazoezi uwanjani hapo na kugundua ubora huo ambao umechagiza kuwawapongeza viongozi wa MREFA, kwa kuutunza vizuri uwanja wa Sokoine.

ìHatuwezi kutaja ni mkoa gani na uwanja gani, lakini wenyewe wanaomiliki viwanja hivyo wanafahamu kwamba viwanja vyao, havistahili kwa maana kwamba havina ubora wa kucheza ligi kuu ya Tanzania Baraî alisema Idd.

Alisema hawana jinsi ya kufanya na viwanja vyenyewe ndivyo hivyo, na klabu ambazo zinatumia viwanja hivyo ndiyo mikoa yao, lazima wavitumie.

Jaffer alisema uwanja wa Sokoine wa mfano kwa maana umetunzwa na unaendelea kutunzwa na MREFA, kwani hata mwaka jana timu yake iliutumia katika michezo yake bado ulikuwa ni mzuri. Amepongeza sehemu ya kucheza mpira ilivyo bora.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.