Yanga yatinga TFF

BURUDANI - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

UONGOZI wa klabu ya Yanga umewasilisha barua kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupinga timu ya Stand United kumtumia mchezaji Frank Igobela.

Yanga ilifungwa 1-0 na Stand United Jumapili iliyopita katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Yanga inadai Stand United imemtumia Igobela kimakosa kwa kuwa bado ni mchezaji halali wa timu ya Polisi ya Zanzibar.

Habari zimeeleza kwamba Yanga imepata taarifa za kutosha kutoka Polisi juu ya mchezaji huyo.

Chanzo hicho, kimedai kuwa Yanga wana ushahidi hadi wa barua ya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kikiizuia TFF kumuidhinisha mchezaji huyo kucheza ligi msimu huu hadi amalizane na Polisi.

Pia, Yanga wanadai Igobela alicheza mechi hiyo, akiwa hana leseni, lakini wamejaribu kufuatilia TFF tangu jana hawajapata majibu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.