Manji ajibu mapigo

BURUDANI - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

TABIA ya kujibu mapigo katika klabu za Simba na Yanga imeendelea kujionyesha tena baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji kuipa klabu hiyo eneo la kujenga uwanja.

Katika kile kinachoonekana msimu huu utakuwa wa kufunikana, Simba hivi karibuni ilianza ujenzi wa uwanja wake katika eneo la Boko, lakini sehemu waliyopata Yanga ya kufanya ujenzi huo ni Kigambo.

Manji ameipa klabu hiyo eneo la ekari 715 ufukweni mwa Bahari ya Hindi, upande wa Geza Ulole, Kigamboni, Dar es Salaam.

Wasaidizi wa Manji walikabidhi eneo hilo jana mchana katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na maofisa wa Chama na Serikali huko Kigamboni.

Aliyepokea eneo hilo kwa niaba ya klabu ni Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa klabu, Mama Fatma Karume aliyekuwa amefuatana na mjumbe mwingine wa Bodi hiyo, Dk. Jabir Katundu, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu, Samuel Lukumay na Kaimu Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mama Karume, mke wa rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Amaan Karume alisema kwamba Baraza lake lilikuwa na kikao na Mwenyekiti wa klabu, Manji kabla ya hatua hiyo.

ìBaada ya wanachama kuomba wenyewe katika Mkutano Mkuu kuwa wanataka Uwanja, sisi tulikaa na Mwenyekiti na tukakubaliana juu ya jambo hili,îalisema.

Hata hivyo, BURUDANI linafahamu kwamba uwanja huo ulikuwa ukabidhiwe juzi au jana lakini ilishindikana kwa sababu zilizoshindikana kutokana na kiongozi mmoja wa serikali aliyepaswa kuweka jiwe la msingi, kubanwa na shughuli nyingine.

Yussuf Manji

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.