Joto kali laiwahisha Serengeti Boys Congo

BURUDANI - - HABARI - NA DEUSDEDIT UNDOLE

TIMU ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, Serengeti Boys, imeondoka nchini jana kwenda Brazzaville, Congo tayari kuwavaa wenyeji Oktoba 2, mwaka huu.

Safari hiyo ni kwa ajili ya Serengeti kucheza mechi ya marudiano ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo, ambazo zitachezwa Aprili, mwakani nchini Madagascar.

Mkuu wa Msafara wa timu hiyo, Ayoub Nyenzi akizungumza Dar es Salaam jana kabla ya kuanza safari, alisema ameamua kwenda mapema ili wachezaji wakazoee hali ya hewa ya huko.

Alisema licha ya Serengeti kuweka kambi ya takriban siku 10 nchini Rwanda, lakini hali ya hewa ya Congo ya joto kali ikilinganishwa na Dar es Salaam. Congo ni nyuzi joto 32 wakati Dar es Salaam ni 29.

Alisema timu hiyo imepangwa kuondoka na wachezaji 19, makocha, daktari na mtunza vifaa.

Akizungumzia mechi hiyo ya marudiano, alisema anaamini vijana wako na ari ya juu ili kuhakikisha wanafanya vizuri na wanafuzu kwenye fainali hizo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.